Picha kwa hisani –
Maafisa wa Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC, wamemtia nguvuni mbunge wa Lari, Jonah Mburu pamoja na Wanakamati watano wa hazina ya CDF eneo bunge hilo kwa madai ya ubadhirifu wa mali ya umma.
Mburu na wenzake wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani siku ya Jumatatu juma lijalo kwa kuhusika na uporaji wa shilingi milioni 27, fedha ambazo zilikuwa zimetengwa na hazina hiyo kufanikisha miradi ya shule na kituo cha michezo.
Kutiwa nguvuni kwa mbunge hiyo kumetokana na agizo kutokana kwa Mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma Noordin Hajj, akihusishwa na sakata ya ufisadi, utumizi mbaya wa ofisi, na kula njama ya kufanya uhalifu wa kiuchumi.
Hata hivyo waliotiwa nguvuni na Mbunge hiyo ni Mwenyekiti wa CDF eneo bunge hilo Peter Mwangi, Mhasibu Ayaan Mahadhi, Karani wa hazina hiyo Francis Kamuyu, na Mwanakandarasi Grace Macharia.