Picha kwa Hisani –
Aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri ya bandari nchini Daniel Manduku amefikishwa mahakama ya milimani kujibu mashata ya ufisadi na utumizi mbaya wa afisi.
Wakiwa mbele ya hakimu Lawrence Mugambi Manduku pamoja na afisa wa halmashauri hio Juma Fadhili wamekanusha madai ya kufuja milioni 244 kwa kuwalipa wanakandarasi kwa kazi ambayo haikukamilishwa.
Hakimu Mugambi hata hivyo ameamuru wawili hao kusalimisha vyeti vyao vya usafiri na kutowasiliana na mashahidi wa kesi hio,na baadae hii leo mahakama itatoa uamuzi kuhusu dhamana ya wawili hao.
Wakati wa kusilikilizwa kwa kesi hio upande wa mashtaka umeitaka mahakama kuwapa dhamana iliokiwango sawa na fedha zilizofujwa,ombi ambalo limepingwa na wakili wa Manduku ,Nelson Havi akisema manduku sio mfanyikazi tena wa halmashauri ya bandari na huenda akashindwa kulipa dhamana ya kiwango kikubwa cha pesa.