Mwanariadha Daniel Kiptum kutoka kaunti ya Nandi alimpiku bingwa mtetezi wa mbio za 21km kwa wanaume Peter Rotich na kutwaa medali ya dhahabu kwenye makala ya tano ya mbio za Safaricom Deaf Marathon zilizoandaliwa hapo jana jumapili katika kaunti ya Mombasa.
Kiptum ambayepia aliwahi kushinda dhahabu kwenye mbio za Sumsun Deaflympic zilizofanyika nchini Uturuki mwaka wa 2017 alitumia muda wa saa moja dakika nane na sekunde 92(1:08:92 )na kuwashinda Martin Gachie na Peter rotich waliomaliza katika nafasi ya pili na tatu mtawalia .
Upande wa wanawake Juster Kwamesa alimshinda Naibin Mushitoi na kujizolea medali ya dhahabu huku, Lucas Wanjiru na Rose Mushitoi wakishinda dhahabu kwenye mbio za 10km upande wa wanaume na wanawake mtwalia .
Washindi kwenye mbio za 21km walitia kibindoni shillingi laki moja mshindi wa pili shillingi 50,000,na mshindi wa tatu akipata shillingi 30,000 huku mshindi kwenye mbio za 10km akijinyakulia shilling 50,000 mshindi wa pili na watatu wakipokezwa kitita cha shilling 40,000 na 30,000.
Taarifa na Cyrus Ngonyo.