Mwanasiasa wa chama cha Jubilee kaunti ya Mombasa Abdi Daib ameihimiza serikali kuu kuibuka na mbinu mbadala ya kukabiliana na deni la kitaifa la shilingi trilioni 5.1.
Daib anasema hatua ya serikali kuwakandamiza wananchi kupitia utozaji wa ushuru wa asilimia 16 kwa thamani ya bidhaa unawanyanyasa wakenya haswa kwa kusababisha kupanda kwa gharama ya maisha.
Kwa sasa lita moja ya mafuta ya petroli jijini Mombasa inauzwa kwa shilingi 124, lita ya mafuta ya diseli ikiuzwa kwa shilingi 110 na mafuta ya taa yakiuzwa kwa shilingi 93 kwa lita.
Taarifa na Hussein Mdune.