Msanii Daddie Selle Abdalla alievuma na kibao Machungu mwaka 2008 amefunguka kuhusu kurudi katika tansia ya mziki.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook msanii huyo amesema hakuna haja kwake kurudi kwani nafasi yake imejaza na mwanamziki Ally Mahaba kwa sasa.
“Ali Mahaba…… huyu mdogo wangu ametisha sana naisi sina sababu zakurudi kwa game cause kazi ameiweza najiona ndani yake kama ulinikubali basi hii ni season 2 Mtoto Wa Mombasani,” ameandika Selle.
Daddy Sele ni mmoja kati ya wasanii wa ukanda wa Pwani waliokuwa na ushawishi mkubwa na nafasi ya kufanya vyema ila alikosa kushikwa mkono na kukuzwa kisanaa.
Taarifa na Dominick Mwambui