Picha kwa hisani –
Wanamuziki wa kikundi cha CSM Wazito kutoka kaunti ya Kilifi, kanda ya Pwani waliachia ngoma yao mpya ambayo walimshirikisha Bandanna inayoitwa ‘Medicine.’
Kikundi hicho kinachojumlisha wasanii Mitindo na Baila, wameonyesha uwezo wao kwa mara ingine tena baada ya kuzindua kazi yao mpya janakupita kipindi cha Kaya Flavaz.
Katika ngoma hiyo, ‘Medicine’ CSM Wazito wamemshirikisha mwanamuziki Bandanna na imetengezwa katika recording label ya Kubwa studios na Producer Grandmaster Teknixx chini ya uongozi wa Rockcity music.
CSM Wazito walivuka chipukizi na ngoma yao ‘Foko’ ambayo ilifanya vyema ndani na nje ya mkoa mwisho wa mwaka jana, kisha wakawachia ngoma ingine miezi minne iliyopita kwa jina ‘Baby’ ambayo mashabiki walionekana kuikubali sana na kufanya vyema kwa stesheni nyingi za Pwani.
Aidha mashabiki wamewasifu sana wasanii wa kikundi hicho na kuutambua uwezo wao kupitia mitandao ya kijamii.
Je, unauzungumziaje muziki unaofanywa na CSM Wazito?