Msanii Confuser J kutoka kaunti ya Kilifi amewashukuru Mungu na watu waliomwokoa baada ya kupata ajali katika eneo la Chumani walipokuwa wanatoka katika tamasha ya Coconut Festival mjini Malindi.
Msanii huyo alipata ajali muda mfupi baada ya kushiriki katika tamasha hilo.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook ameandika: “Jamaa tumepata ajali mbaya chumani dereva wangu amekatika vidole..mm nimumia mkono kichwa kidogo na kifua..tunaenda hospital saa hii..tumekosa matibabu chumani.. Asante mungu kwakutunusuru”
Wawe pole wote