Picha Kwa Hisani –
Msanii wa Bongofleva, Harmonize ameweka wazi jina la wimbo ambao wameimba na mwanamuziki kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Awilo Longomba kuwa ni ‘Attitude’ na kutaja siku utakaoachiwa.
Harmonize amedokeza hayo mchana wa leo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo alichapisha picha inayowaonyesha wasanii aliowashirikisha.
Mbali na Longomba, Harmoze amemshirikisha mkongwe wa muziki wa Bolingo, H.Baba.
Aidha ameeleza siku ya kuuachia wimbo huo kuwa itakuwa Ijumaa hii ya Aprili 23, 2021.
Harmonize ametumia nafasi ya Awilo kuwepo nchini akiwa anarekodi filamu ya ‘A life to Regret’ kufanya shughuli hiyo.
Mbali na Harmonize, Awilo alieleza kuna wasanii wengine ambao ataingia nao studio ambao hakuwa wazi kuwataja.