Picha Kwa Hisani –
ATL Music wamesitisha collabo ya mwanamuziki tajika kutoka Mombasa ambaye yupo chini ya usimamizi wao Ally Mahaba na msanii wa Bongo fleva Aslay Isihaka.
Usimamizi wa ATL umechukua uamuzi huo baada ya kubaini kuwa mafisa wa polisi nchini humo wamearishwa kumkamata Ally Mahaba baada ya kubainika kuwa alimpachika mimba mtoto wa afisa mmoja mwenye ushawishi katika serikali ya Tanzania mjini Dar Es Salaam.
Ally Mahaba alistahili kuondoka nchini kuelekea Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya video ya ngoma hiyo lakini ilani ya kukamatwa kwa Ally Mahaba imepelekea Meneja wake anayejulikana kwa jina Martin kusitisha safari hio kwa sasa.
“Kijana wangu na timu yake ilifaa kuelekea Tanzania lakini hizi report zimeharibu mipango kabisa siwezi kuruhusu Ally aingie Dar kabla sijabaini ni nini kinaendelea” amesema Martin
Aidha, meneja huyo yuko tayari kushirikiana na maafisa wa Usalama endapo repoti hio itawasilishwa kwa mafisa wa usalama nchini Kenya.