Coast Stima imetoka sare tasa dhidi ya Isibania kwenye mechi ya ligi ya NSL.
Kulingana na meneja wa timu ya Coast Stima walikuwa na nafasi nyingi za kuongeza kwenye mechi hiyo lakini bahati haikuwa upande wao.
” Tulikuwa na nafasi nyingi sana ambazo tungeweza kufunga lakini makali yetu katika safu ya mashambulizi yalikuwa butu,” amesema Kenneth Onuhu.
Onuhu ameongezea kuwa wanalenga kuimarisha safu yao ya mashambulizi kabla hawajakutana na Kangemi tarehe 17 mwezi huu.
Klabu ya Coast Stima ipo na pointi 34 baada ya mechi 26.
Kwenye matokeo ya mechi zingine zilizochezwa Jumapili.
Kibera Black Stars 1-1 Nairobi City Stars
Nairobi Stima 2 -1 Ushuru FC
Taarifa na Dominick Mwambui.