Baada yakufahamika kama Rais wa mziki wa kizazi kipya kwa muda mrefu sasa Msanii Jackson Makini amejiita mfalme.
Kupitia kwa kibao kinachoitwa “King” alichokitoa leo, Prezzo amedai kuwa yeye ndiye mfalme kwa mabadiliko aliyoyaleta katika tasnia ya mziki wa kizazi kipya.
Kwenye wimbo huu amezungumzia kuhusu jinsi alivyoruka kwa Chopper hadi katika ukumbi ulioandaa tuzo za Chaguo La Teeniz. Kwenye tuzo hizo Prezzo aliteuliwa kwenye vitengo 7.
Prezzo ni mmoja miongoni mwa wasanii walioleta mwamko wa mziki wa kizazi kipya humu nchini.
Tazama wimbo huo hapa>>>https://www.youtube.com/watch?v=Df6nip2Ym0U
Taarifa na Dominick Mwambui.