Katibu mtendaji wa Baraza la Maimamu na Wahubiri wa humu nchini CIPK sheikh Mohamed Khalifa amesema kuwa kuzembea kwa wazazi katika majukumu yao ya ulezi sawia na kukithiri kwa utumizi wa mihadarati miongoni mwa vijana ndio chanzo kikuu cha utovu wa usalama kaunti ya Mombasa.
Kulingana na Khalifa wazazi wengi katika kaunti hiyo wamesahau majukumu yao ya ulezi hali ambayo imewaacha vijana wengi kupotoka kimaadili na kujihusisha na vitendo vinavyoathiri usalama.
Kiongozi huyo wa kidini amesema kuwa wazazi wakiwajibikia kikamilifu majukumu yao visa vya utovu wa usalama katika kaunti ya Mombasa vitakabiliwa.
Taarifa na Cyrus Ngonyo.