Story by Bakari Ali-
Usimamizi wa chuo kikuu cha Moi nchini umekanusha madai yaliyoibuliwa kwamba chuo hicho kimeajiri wafanyakazi hewa kwa lengo la kufuja mali ya umma.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa kwenye kongamano la kuweka mikakati ya kuboresha chuo hicho, Mwenyekiti wa baraza la chuo hicho Dkt Kimani Njuguna amepinga madai hayo akisema usimamizi wa chuo hicho haujahusika na maswala kama hayo.
Dkt Kimani ameweka wazi kwamba usimamizi wa chuo hicho unafanya kila juhudi kuboresha chuo hicho ili kiwe miongoni mwa vyuo vikuu bora katika kanda ya Afrika Mashariki na haipaswi kuwekewa madai ya uongo ambayo yanaweza kuathiri hadhi ya chuo hicho.
Kwa upande wake, Naibu Chansela wa chuo hicho Prof Isaac Sang ameitaka serikali kushirikiana na chuo hicho katika kuweka mikakati ilitakayoboresha sekta ya elimu, teknolijia na ukulima nchini.