Chuo kikuu cha kiufundi cha Mombasa TUM kimefungwa baada ya usimamizi wa chuo hicho kuafikiana kufuatia athari ya virusi vya Corona humu nchini.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliotiwa saini na Naibu Chansella wa chuo hicho Prof Laila Abubakar ni kwamba,chuo hicho kilicho na zaidi ya Wanafunzi elfu 15 kiko hatarini kukumbwa na maambukizi.
Wanafunzi wote wameamrishwa kuondoka chuoni humo hii leo na kusafiri nyumbani kwao na kusubiri tangazo rasmi la kurudi chuoni humo pindi hali itakapokuwa shwari nchini.
Hatua hiyo imeathiri mitihani ya katikati ya muhula iliyoanza mapema hii leo, sawia na uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Wanafunzi TUMSA uliyopaswa kufanyika hii leo japo ukasitishwa punde tu baada ya Wanafunzi kupanga foleni wakisubiri kupiga kura.