Picha kwa hisani –
Serikali ya kaunti ya kwale imesema chuo cha kutoa mafunzo kwa walimu cha Bang’a kilichoidhinishwa na serikali ya kaunti hiyo kinatarajiwa kuanza kutoa mafunzo rasmi hapo mwaka ujao.
Gavana wa kaunti hiyo Salim Mvurya amesema serikali kuu imeweza kutoa shilingi milioni 150 zitakazotumika katika kumalizika kwa ujenzi wa chuo hicho ili kianze kutoa mafunzo.
Wakati uo huo ametaja kukamilika kwa chuo hicho kama hatua kubwa kwa kaunti ya kwale katika masuala ya elimu kutokana na kuwa kaunti inayoongoza nchini katika masuala ya elimu.