Picha kwa hisani –
Chris Brown amekataa jina lake na uwezo wake kulinganishwe na mtu yeyote hapa duniani, jambo lililomsababisha amjibu kwa maneno makali shabiki mmoja ambaye alilinganisha uwezo wake na mchezaji wa NBA, Ben Simmons.
Shabiki huyo aliandika kupitia twitter kwamba Chris Brown na R&B yake ni kama Ben Simmons kwenye Kikapu. Yani hakuna maendeleo yoyote wala hatua anayopiga, hashuki, yuko vile vile, ni msanii wa hivyo tu.
Breezy alimshushia maneno makali shabiki huyo akitaka asimchezee hata kidogo na asimlinganishe na mtu yeyote. Kubwa zaidi alimwambia “Sasa nenda kamuulize mama yako, yupi ni baba yako halisi.”