Mtayarishaji wa mziki Chizan Brain amefunguka na kusema kuwa utumizi wa kiki katika tasnia ya mziki ni mzuri.
Mwanamziki huyo ambaye aliwahi kuwa katika kundi la Ukoo Fulani hapa Mombasa miaka ya nyuma amesema kuwa mziki ulipofika unahitaji kuuzwa kwa njia mbalimbali ili kuweza kufikia sikio la msikilizaji.
Kulingana naye mziki sasa umekuwa mwingi na nafasi ni ndogo katika vyombo vya habari hivyo basi wasanii wanafaa kuibuka na mbinu za kulinasa sikio la shabiki.
Je unadhani utumizi wa kiki katika mziki ni sawa?