Story by Mwanaamina Fakii –
Mgombea wa kiti cha uwakilishi wa Kike katika kaunti ya Kwale Zainab Chitsangi ameahidi kupigania nyongeza ya mgao wa fedha katika hazina ya NGAAF iwapo atachanguliwa.
Chitsangi amesema mgao huo ni mchache mno na iwapo utaongezwa basi utawajenga uwezo wanawake wengi nchini sawa na kupigania haki zao.
Akizungumza na Wanahabari, Chitsangi amesema yuko tayari kushirikiana na vijana na wanawake katika kuwajenga uwezo akihoji kwamba wakati umefika sasa kwa viongozi wa kike kupewa nafasi ya uongozi.
Wakati uo huo ameihimiza jamii kudumisha amani na utangamano wakati huu ambapo wakenya wanajiandaa kwa uchaguzi mkuu huku akiwatahadharisha wananchi dhidi ya kuchochewa kisiasa.