Story by Our Correspondents –
Aliyekuwa Afisa mkuu mtendaji wa Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC Ezra Chiloba ameteuliwa kuwa mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya mawasiliano nchini CA.
Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo Kembi Gitura amesema Chiloba atashikilia nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka minne.
Taarifa hiyo imesema uteuzi wa Chiloba umejiri baada ya aliyekuwa mkurungezi mkuu wa Mamlaka hiyo Francis Wangusi kustaafu na nafasi hiyo kusalia wazi kwa mda.