Story by Mwanaamina Fakii –
Zaidi ya watahimiwa elfu nane wa kidato cha nne KCSE kutoka kaunti ya Kwale wameanza rasmi mitihani yao ya kitaifa.
Kulingana na Mkurugenzi wa elimu katika kaunti hiyo Martin Cheruiyot, vituo 105 vya mitihani vimetengwa na idara ya elimu ili kuwawezesha watahiniwa hao kufanya mitihani hiyo.
Cheruiyot amesema matokea ya mitihani ya kidato cha nne yatatolewa kabla ya mwezi wa tano hatua ambayo itawapa fursa wanafunzi waliofanya vyema katika mitihani hiyo kujiunga na vyuo vikuu.
Wakati uo huo amewahimiza wazazi kuwajibikia majukumu yao ya ulezi kwa kuhakikisha wanawapa mafunzo ya nidhamu watoto wao wakati wakiwa nyumbani sawa na kuwasaidia kazi za nyumbani.