Story by Salim Mwakazi –
Idara ya elimu kaunti ya Kwale imesema idadi kubwa ya shule za kaunti ya Kwale zimeorodhesha matokeo bora zaidi katika mtihani wa KCSE mwaka wa 2020 ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
Mkurugenzi wa Elimu kaunti ya Kwale Martin Cheruiyot amesema matokeo hayo yameimarika licha ya shule za upili za kaunti ya Kwale kukosa alama ya A katika mtihani huo.
Cheruiyot ameipongeza shule ya upili ya Kwale High iliorodhesha alama wasitani 7.74 na ile ya wasichana ya Matuga iliopata alama wastani 7.09, amesema shule hizo kaunti ya Kwale zimerekodi matokeo ya kuridhisha katika mtihani huo wa kitaifa.
Wakati uo huo amesema japo janga la Corona liliathiri pakubwa shughuli za masomo na kuchangia mda mchache wa wanafunzi kudorusu vitabu vyao, wanafunzi wamejiribu mno.