Story by Our Correspondents-
Rais William Ruto amewasimamisha kazi kwa mda makamishna wanne wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC baada ya bunge la kitaifa siku ya Alhamis kuidhinisha ripoti ya kutimuliwa afisi kwa makamishna hao.
Katika gazeti rasmi la serikali, Rais Ruto amezingatia kipengele cha 145 cha katiba na kuwasimamisha kazi kwa mda makamishna hao ambapo ni pamoja na Naibu Mwenyekiti wa IEBC Juliana Cherera, Kamishna Irene Masit, Justus Nyang’aya na Francis Wanderi.
Rais Ruto amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufaa Aggrey Muchelule kuwa mwenyekiti wa jopokazi la watu 5 ambao watachunguza shtuma ambazo makamishna hao wanakabiliwa nazo.
Hata hivyo wanachama wa jopokazi hilo ni pamoja na Carolyne Daudi, Linda Kiome, Mathew Nyabena na kanali mstaafu Khamis Saed, kisha baadaye jopokazi hilo liwasilishe ripoti kwa rais.