Kikundi kinachojishughulisha na masuala ya kitamaduni maarufu Chendachenda katika kaunti ya kwale kimeendeleza ugavi wa barakoa kwa wafanyabiashara katika soko la kwale ili kudhibiti maambukizi ya korona.
Akizungumza na wanahabari balozi kikundi hicho Grace Mbeyu mumba amesema hatua hiyo ni kutokana na hofu ya kuongezeka kwa visa vya maambukizi ya virusi vya korona nchini.
Amesema wamechagua kutoa barakoa hizo katika masoko ikilinganishwa kwamba hayo ndiyo maeneo ambayo watu wengi hutangamana.
Hata hivyo Mbeyu amewaomba wafadhili mbalimbali kujitokeza na kuwasaidia ili waweze kufikia maeneo mengine yaliyobaki katika kaunti ya kwale.
Soko la kwale ni soko la pili kupata msaada huo wa barakoa kutoka kwa kikundi hicho baada ya soko lile la Calipso eneo la Ukunda.
Kamati ya kitaifa inayosimamia mpango wa kazi vijijini ulioidhinishwa hivi majuzi imezuru kaunti ya kwale ili kukagua shughuli za mradi zinavyoendelea.
Akizungumza na wanahabari katika majengo ya kaunti katibu mkuu katika wizara ya usalama wa ndani nchini Kang’ethe Thuku amesema mpango huo ulibuniwa ili kuwapa vijana fedha za kumudu gharama ya masiha.
Kang’ethe amesema mradi huo pia ulipania kuweka usafi wa mazingira katika vijiji katika kupamabana na maambukizi.
Aidha amesema kufikia sasa takriban milioni 10 zimeweza kuingia katika uchumi huko masinani kutokana na mradi huo.