Story by Our Correspondents –
Mwenyekiti wa Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC, Wafula Chebukati amesema tume hiyo imejiandaa vyema kuanza zoezi la kuwasajili wapiga kura wapya mwezi huu wa Januari.
Chebukati amedokeza kwamba tayari Tume hiyo imepokea pesa za kufanikisha zoezi hilo kutoka kwa hazina ya kitaifa na zoezi hilo litaanza hivi karibu hasa mwezi huu.
Katika kikao na Wanahabari jijini Nairobi, Chebukati amesema wanatarajia kuwasajili wapiga kura wapya milioni 4.5 huku akiwahimiza wakenya ambao bado hawajajisajili kama wapiga kura kutumia zoezi hilo kujisajili.
Wakati huo amewahimiza wakenya kutopuuza zoezi hilo kwani ndio njia pekee ya kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika zoezi la uchaguzi mkuu ujao huku wale ambao hawana vitambulisho vya kitaifa wakihimizwa kuchukua vitambulisho vyao.