Story by Our Correspondents-
Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imeanza zoezi la kupiga msasa sajili ya wapiga kura, siku 96 kabla ya uchaguzi mkuu kuandaliwa mwezi Agosti 9.
Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amesema tume hiyo imeanzisha zoezi hilo ili kubaini kama sajili hiyo iko sawa huku akiwataka wananchi kuhakikisha majina yao katika sajili hiyo yamesajiliwa sawa.
Chebukati amesema zoezi la usajili wa wapiga kura kwa sasa limesitishwa kwa mda hadi tarehe 23 mwezi Machi mwaka wa 2023 kulingana na tangazo rasmi la gazeti la serikali la tarehe 28 mwezi Aprili mwaka wa 2022.
Wakati uo huo ameweka wazi kwamba tume hiyo imejiandaa vyema kuhakikisha inafanikisha uchaguzi huru na haki huku akiwataka wakenya kushirikiana na maafisa wa tume hiyo wa nyanjani.