Story by Our Correspondents –
Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imewahakikishia wakenya kwamba itaandaa uchaguzi huru na haki wakati uchaguzi huo utakapoandaliwa mwezi Agosti mwaka wa 2022.
Mwenyekiti wa Tume hiyo Wafula Chebukati amesema makamishna wa IEBC wamejipanga vyema kuhakikisha uchaguzi huo utaandaliwa bila changamoto zozote huku akiishinikiza serikali kuitengea tume hiyo fedha kwa wakati.
Katika kikao na Wanahabari mjini Mombasa, Chebukati ameitaka idara ya usalama kushirikiana na makamishna wa IEBC ili kuhakikisha uchaguzi huo unaandaliwa kwa amani huku akiwataka wale ambao hawajajisajili kama wapiga kura kujitoza na kujisajili.
Wakati uo huo amewataka wanasiasa kukoma kuendeleza siasa za migawanyiko nchini, akisema siasa hizo zimechangia hofu miongoni mwa wananchi na kuwataka wanasiasa kuwa na subra hadi wakati wa kampeni za kisiasa.