Story y Mimuh Mohamed –
Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC Wafula Chebukati amefika mbele ya kamati ya bunge la kitaifa kuhusu sheria kueleza kuhusu sheria ya kudhibiti fedha zitakazotumika katika kampeni za uchaguzi mkuu.
Chebukati amekuwa na kibarua kigumu kujibu maswali ya wanachama wa kamati hiyo waliomtaka kueleza kwa nini alichapisha muongozo wa fedha za kampeni zitakazotumiwa na wagombea kabla ya mswada huo kuidhinishwa na bunge.
Chebukati kwenye maelezo yake amesema sheria ya fedha za kampeni za uchaguzi ya mwaka 2013 inahitilafu ndiposa tume hiyo ikawasilisha mswada kuhusu sheria hiyo mnamo tarehe 21 mwezi Agosti mwaka 2020 lakini bunge lilikosa kuuidhinisha.
Wanachama wa kamati hiyo wameelezea kutoridhishwa kwao na hatua ya IEBC ya kuchapisha muongozo wa fedha za kamapeni siku ya Jumatatu juma hili kabla ya bunge kuidhinisha mswada huo,wakisema hatua hiyo ililenga kuonyesha wakenya kwamba bunge limefeli kutekeleza majukumu yake.