Shirika la kutetea haki za binadamu la HURIA limesema kuwa ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana umepelekea wengi wao kujitosa kwenye utumizi wa mihadrati.
Akiongea katika kikao cha kuhamasisha jamii katika eneo la Malindi, afisa wa shirika hilo Antony Maganga, amesema kuwa hatua hiyo imewafanya vijana kukosa matumaini ya kimaisha na hatimaye kujiingiza kwenye utumizi wa mihadarati.
Maganga vile vile amewashauri wazazi wa hapa pwani kushirikiana na viongozi katika maeneo yao ilikuhakikisha kwamba wanabuni mikakati ya kuwanasua vijana kutokana na janga hilo la mihadarati.
Taarifa na Esther Mwagandi.