Story by Gabriel Mwaganjoni –
Vyama vitatu vya kisiasa kutoka ukanda wa Pwani ikiwemo chama cha Kadu Asili, Umoja Summit na Shirikisho vimetia saini mkataba wa kubuni Muungano wa kisiasa unafahakamika kama Ukombozi wa Majimbo.
Mwenyekiti wa kitaifa wa Chama cha Umoja Summit Matano Kheri amesema tayari Muungano huo wa kisiasa unaendeleza mazungumzo na chama cha PAA sawa na kuwahamasisha wapwani kuhusu malengo ya Muungano huo.
Katika mkao na Wanahabari katika kaunti ya Mombasa, Matano amesema ni sharti wapwani wafungukwe na macho na kujipanga kisiasa jinsi maeneo mengine ya nchi yanavyojipanga.
Kwa upande wake Kinara wa Chama hicho cha Umoja Summit Patrick Birya amesema maswala ya ardhi, haki za kibinadamu, dhuluma za kihistoria ni baadhi tu ya agenda kuu za Muungano huo.