Story by Our Correspondents-
Kinara wa chama cha UDA ambaye pia ni Naibu Rais Dkt William Ruto amewahimiza wagombea wote wa viti mbalimbali vya kisiasa watakaoshiriki kura za mchujo wa chama hicho tarehe 14 mwezi huu kudumisha amani.
Katika kikao na Wanahabari jijini Nairobi, Ruto amesema tayari chama hicho kimesambaza vifaa ya kupigia kura katika kaunti 35 kote nchini ambazo zitashiriki kura hizo za mchujo, huku akisisitiza haja ya wafuasi wa chama hicho kudumisha amani.
Ruto ameahidi kwamba zoezi hilo kote nchini litakuwa huru na haki kwa wagombea na wafuasi wao ili kuzuia kushuhudiwa kwa sintofahamu za kisiasa na mivitano isiyokuwa na msingi wowote.
Hata hivyo tayari baadhi ya wagombea wamepewa tiketi ya moja kwa moja ya chama hicho akiwemo Hassan Omar Sarai anayelenga kiti cha ugavana wa Mombasa, Mohamed Ali kiti cha ubunge wa Nyali, Karisa Nzai- Jomvu, Omar Shallo -Mvita, na Hamis Mwaguya anayelenga kiti cha useneta wa Mombasa.