Story by Hussein Mdune –
Chama cha ODM kaunti ya Kwale kimemchagua tena Mwanasiasa Hassan Mwanyoha kama Mwenyekiti wa chama hicho kaunti ya Kwale.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kukamilika kwa uchaguzi huo, Mwanyoa ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Matuga amesema uchaguzi huo umefanywa kwa kuzingatia muongozo wa chama na Katiba.
Naye mshirikishi wa chama hicho kaunti ya Kwale Nicholas Zani amesema watahakikisha wanaendeleza hamasa kwa wakaazi wa mashinani kuhusu umuhimu wa kujisajili kama wapiga kura.
Kwa upande wake Najma Mwandoto ambaye ni Mwakilishi wa vijana katika chama hicho kaunti ya Kwale amewataka wakaazi wa Kwale kushirikiana na kutokubali kutumiwa kisiasa.
Katika uchaguzi huo Hassan Mwanyoha amechaguliwa kama Mwenyekiti, Naibu Mwenyekiti akichaguliwa Shaban Luchesi, Katibu akichaguliwa William Opondo, Mshirikishi wa chama hicho Nicholas Zani miongoni mwa wengine.