Story by Bakari Ali –
Wanachama na viongozi wa chama cha ODM katika kaunti ya Mombasa wamehimizwa kuendeleza hamasa kwa wakaazi wa kaunti hiyo kuhusu kujisajili kama wapiga kura.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kuwapokea wanasiasa walioasi vyama mbalimbali nchini na kujiungana na chama cha ODM, Mwenyekiti wa chama hicho kaunti ya Mombasa Mohammed Hamid Khamis amesisitiza umuhimu wa wakaazi kujisajili kama wapiga kura.
Hamid amesema ni wazi kwamba chama cha ODM kingali imara katika kaunti ya Mombasa baada ya wanasiasa hao kujiunga na chama hicho huku wakipania kuendelea kukikuza chama hicho.
Kwa upande wake Katibu mkuu wa chama cha ODM kaunti ya Mombasa Geoffrey Busaka amesema chama hicho kinameweka mikakati mwafaka kuhakikisha kaunti ya Mombasa inashuhudia uchaguzi wa amani.