Story by Our Correspondents-
Mgombea wa kiti cha ugavana katika kaunti ya Kwale Prof Hamadi Boga amewashukuru wakaazi wa kaunti ya Kwale, wanachama wa ODM na kamati ya kitaifa ya uchaguzi katika chama hicho kwa kumkabidhi tiketi ya moja kwa moja ya chama hicho.
Katika mahojiano ya kipekee na kituo cha Radio Kaya, Boga amesema hatua hiyo imeonyesha wazi kwamba chama hicho kina imani na uongozi wake huku akiahidi kuzuru mashinani na kumpigia debe Odinga kuingia Ikulu.
Kiongozi huyo hata hivyo amewarai wakaazi wa kaunti ya Kwale kujitenga na siasa za vurugu na ukabila na badala yake kuwa mstari wa mbele kuhubiri amani sawa na kuwachagua viongozi wenye malengo ya maendeleo.
Wakati uo huo ameahidi kuhakikisha swala la uhaba wa maji katika kaunti ya Kwale linapata suluhu la kudumu huku akisema uboreshaji wa mikakati endelevu itakabiliana na changamoto za baa la njaa na ukame kaunti ya Kwale.
Asante Gavana Mtakiwa kaunti ya Kwale