Huku mgogoro ukiendelea kushuhudiwa ndani ya chama cha Jubilee, baadhi ya viongozi wa vyama tanzu katika chama hicho sasa wanashinikiza kivunjwe.
Akiongea mjini Kwale aliyekuwa kiongozi wa chama cha TipTip Kalembe Ndile, amemtaka rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto, kuvunja chama hicho akisema kuwa kimepoteza mwelekeo.
Kalembe amesema kuwa licha ya Rais Kenyatta kuwaonya baadhi ya viongozi wakuu wa chama hicho dhidi ya kuendeleza kampeni za mapema kuhusu uchaguzi wa mwaka wa 2022, viongozi hao wamekaidi onyo la Rais.
Kalembe amepuuzilia mbali mkataba wa urithi wa kiti cha urais kati ya Kenyatta na Ruto, akisema kuwa viongozi wa vyama tanzu vya Jubilee hawakukubaliana juu ya suala hilo.
Taarifa na Michael Otieno.