Picha kwa hisani –
Siku moja tu baada ya Naibu Rais Dkt William Ruto kuandaa mkutano ndani ya afisi za makao makuu ya Chama cha Jubilee, Sasa Kamati simamizi ya chama hicho inalitaka Baraza kuu la chama cha Jubilee kumtimua Ruto chamani.
Katibu mkuu wa Chama hicho Raphael Tuju, amesema hatua hiyo imetokana na jinsi Ruto anavyoenda kinyume na muongozo wa chama sawia na kuwaunga mkono wabunge waliokosa heshima na kumdhalilisha Mama Ngina Kenyatta na familia yake.
Katika kikao na Wanahabari nje ya afisi za makao makuu ya chama hicho kule Nairobi, Tuju amesema uongozi wa jubilee hauwezi kumruhusu Ruto kuendelea kukaidi ushauri wa Kinara wa chama hicho Rais Uhuru Kenyatta, kwani hatua hiyo ni sawa na mapinduzi ya chama.
Tuju amesema Kamati hiyo ameafikia kuamuzi huo sawia na kumkataza Ruto kufika katika afisi hizo na kufanya mikutano ya kisiasa ya mwaka 2022 kwani kiongozi huyo amekosa muelekeo na kuenda kinyume na matarajio ya rais.