Story by Gabriel Mwaganjoni
Chama cha Jubilee kimesema kitafanya kila juhudi ili kuhakikisha mrengo wa Azimio la Umoja unaunda Serikali baada ya uchaguzi wa Agosti, 9.
Mwenyekiti wa kitaifa wa chama hicho Nelson Dzuya amesema chama hicho kimejiweka katika nafasi ya kuunda tena Serikali kikishirikiana na vyama tanzu vya kisiasa ndani ya mrengo huo wa Azimio la Umoja-One Kenya.
Akizungumza katika eneo bunge la Jomvu kaunti ya Mombasa, Dzuya amesema ni sharti chama hicho kionyeshe uwezo na ukakamavu wake wa kuunda Serikali katika uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti kwa kufanya kampeni katika kila pembe ya nchi.
Dzuya vile vile amekariri kwamba atawaongoza wagombea wa viti mbalimbali vya uongozi na wafuasi wa chama hicho katika kuendeleza kampeni za kisiasa hapa Pwani.