Picha kwa hisani –
Mawakili wa kiongozi wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine wamewasilisha kesi katika mahakama ya juu zaidi wakitaka Rais Museveni azuiwe kushiriki uchaguzi ujao.
Wakili wa Bobi Wine Medard Ssegona alipokuwa akiwasilisha kesi hiyo alisema kuwa hawataki kumona Yoweri Kaguta Museveni akishiriki tena uchaguzi ambapo alimshutumu kupanga ghasia.
Awali naibu mwenyekiti wa chama cha NUP, John Batst Nambesh ambaye pia ni naibu mwenyekiti mkoa wa mashariki alidai wana ushahidi wa kutosha kuonyesha udaganyifu uliofanyika katika uchaguzi uliopita nchini humo.
Wagombea wengine wa Urais pia wamejitokeza kupinga wazi matokeo ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na Patric Amuriat wa chama cha FDC, Jenerali Mugisha Muntu wa chama cha ANT, Norbert Mao wa chama cha DP na mgombea huru Jenerali Henery Tumukunde.