Picha kwa Hisani –
Idara ya usalama imeteketeza chakula chenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10 katika kaunti ya Mombasa.
Mshirikishi mkuu wa utawala Kanda ya Pwani John Elungata amesema chakula hicho ni mchele na tambi maarufu spaghetti na kilibainika kuwa sio salama kwa matumizi ya binadamu.
Elungata amesema chakula hicho kiliingizwa nchini kutoka nchini Utaliano kupitia bandari ya Mombasa mwaka wa 2018.
Elungata hata hivyo amesema licha ya kunasa makasha hayo katika mabohari tofauti eneo la Changamwe na Shimanzi,wamiliki wake hadi sasa hawajapatikana kwa kipindi hicho cha miaka miwili.
Elungata amesisitiza kwamba upekuzi zaidi katika mabohari yote ya uhifadhi shehena umeimarishwa akihoji kwamba pindi mali bandia inayoingizwa humu nchini itakaponaswa itaharibiwa.