Na: Rasi Mangale.
Celtic FC ndio mabingwa wa makala ya Msambweni kwa watoto wasiozidi umri wa 13 baada ya kuitandika Bomani Youth kwa njia ya matuta kwenye michuano ya siku moja iliyochezwa uga wa Chibubu Msambweni.
Celtic walizawadiwa kikombe na mipira miwili huku Bomani youth wakipata mipira miwili.
Lengo la michuano hii lilikuwa ni kuwahamsisha watoto dhidhi ya matumizi ya mihadarati, kukuza talanta na kuwajenga kimaadali.
Makala haya yaliandaliwa na shirika la SambaSports youth Agenda ,Radio Kaya na ushirikiano wa BaseTitanium.