MGOMO: Wauguzi wafutilia mbali mgomo wao uliodumu kwa takribani siku 79 na kurejea kazini
Picha kwa hisani –
Muungano wa wauguzi nchini umefutilia mbali mgomo wao uliodumu kwa takribani siku 79 na kutangaza kurejea kazini.
Katibu mkuu wa Muungano huo nchini Seth Panyako, amesema Muungano huo umechukua hatua hiyo baada ya kupkea agizo la Mahakama kwamba wanafaa kusitisha mgomo wao huku wakiendelea na mazungumzo.
Panyako amewaagiza Wauguzi wote nchini kurejea kazini mara moja, huku viongozi wa Muungano huo wakiendeleza mazungumza ya kuafikia mkataba wa maelewano kati ya viongozi wa serikali, zile za kaunti ya Muungano huo.
Siku ya Jumatato, Jaji wa Mahakama ya Leba Maureen Onyango, aliagiza kusitishwa kwa mgomo wa Wauguzi na kurejea kazini mara moja huku akiziagiza serikali za kaunti kusitisha adhabu waliokuwa wamepanga kuwapa wauguzi nchini.