Kituo cha habari cha Radio Kaya, kimesambaza vifaa vya kujikinga na maambukizi ya Corona kwa wafungwa
Idara ya usalama katika kituo cha polisi kwa Kwale, imekishukuru kituo cha habari cha Radio Kaya kwa juhuzi zake za kukabiliana na janga la Corona sawia na kuihamaisha jamii kuhusu umuhimu wa kuzingatia masharti ya kiafya.
Akizungumza baada ya kupokea misaada mbalimbali ikiwemo Sabuni kutoka kwa watangazaji wa Radio Kaya, Afisa mkuu polisi anayesimamia kituo cha polisi cha Kwale, Ludwin Sasati, amewahimiza wakaazi kuzingatia masharti hayo.
Sasati pia ameyahimiza mashirika mbalimbali ya kijamii kujitokeza na kuwasaidia vijana katika kuwabunia ajira ili kuzuia wengi wao kujihusisha na utovu wa usalama.
Wakati uo huo amedokeza kuwa zaidi ya watu 200 katika kaunti ya Kwale wameshtakiwa kwa kutozingatia masharti yaliowekwa na Wizara ya Afya nchini ya kudhibiti maambukizi, akisema ni lazima watu wawe waangalifu.
Mbali na kituo hicho cha polisi cha Kwale, vile vile gereza la Wanawake la Kwale limeweza kupokea misaada hiyo ili kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona.