
Wahudumu wa uchukuzi wa umma waonywa vikali-Lungalunga
Wahudumu wa matatu katika eneo bunge la lungalunga kaunti ya kwale wamehimizwa kukoma kukiuka maagizo ya serikali katika kudhibiti janga la korona nchini wanapokua barabarani.
Afisa mkuu wa polisi eneo hilo Peter Nzimbi amesema maafisa wa usalama eneo hilo wamegundua kwamba wahudumu hao wamebuni mbinu mbalimbali za kukiuka maagizo hayo ikiwemo kupitia ushirikiano na wahudumu wa bodaboda wanapokaribia vizuizini.
Amesema wahudumu hao hushukisha idadi ya abiria waliopita kiwango hitajika katika matatu na kushirikiana na wahudumu wa bodaboda katika kuwavukisha vizuizi vya usalama akisema yeyote atakayekamatwa akiendeleza tabia hiyo atakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.