Ralph Sandal Masai maarufu kama Cannibal amekanusha madai kuwa aliokoka ili kusaka pesa katika soko la mziki wa injili.
Kulingana na msanii huyo ni kuwa aliokoka kwa sababu ya imani yake na wala sio kwa sababu ya pesa.
“Nimeambiwa ati jamaa amebadilisha imani kwa sababu ya kakitu. Watu wanongea ongea lakini am not here for the money, am here for the word and gospel. Kwa sababu maandiko pia yanasema seek ye first the kingdom of God and all shall be added unto you. So first am on the kingdom, I want to manifest the gifts of the Holy Spirit because that is priceless,” ameandika msanii huyo kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Taarifa na Dominick Mwambui.