Taarifa na Charo Banda
Siku chache baada ya kanisa la Malindi Deliverance kubomolewa sasa bwenyenye mmoja amejitokeza na kudai kwamba ndie mmiliki halisi wa kipande hicho cha ardhi kilichojengwa kanisa hilo.
Akiongea na wanahabari bwenyenye huyo kwa jina Japhet Noti Charo amesema kuwa usimamizi wa kanisa hilo uliomba sehemu ya ardhi hio kufanya idaba zao kwa muda tu kabla ya kujengwa kanisa hilo.
Noti aidha amesema kuwa ubomozi wa Kanisa hilo umetokana na agizo la mahakama la kuwataka waumini hao kuondoka katika eneo hilo akisema huenda usimamizi wa kanisa hilo ulikua na njama ya kunyakua kipande hicho cha ardhi cha ekari moja.
Hata hivyo Kasisi wa kanisa hilo Paul Mutunga anadai kuwa haukupewa taarifa yoyote ya mahakama kuhusu ubomozi wa kanisa hilo huku viongozi mbali mbali wa kidini wakishtumu vikali hatua hiyo wakisema kuwa sehemu zote za kuabudu zinastahili kuheshimiwa.