Story by Our Correspondents –
Mali ya thamani isiojulikana imeteketea baada ya bweni la shule ya upili ya Golini eneo la Matuga kaunti ya Kwale kushika moto.
Kulingana na walioshuhudia mkasa huo, huenda moto huo umesababishwa na hitilafu za nguvu za umme japo juhudi za wakaazi kuuzima moto huo hazikufaulu kwani wazima moto kutoka kaunti ya Kwale walifika kuchelewa katika eneo la tukio.
Afisa wa polisi anayesimamia kituo cha polisi cha Kwale Phillip Ngatia amethibitisha kutokea kwa mkasa huo na kudai kwamba tayari uchunguzi umeanzishwa japo hakuna mwanafunzi yeyote aliyejeruhiwa.
Wakati uo huo bweni la shule ya upili Dkt Kraft katika eneo la Rabai kaunti ya Kilifi limeteketea baada ya kutokea hitilafu za nguvu za umme.