Picha kwa Hisani –
Hatimaye aliyekuwa rais wa tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin William Mkapa amezikwa nyumbani kwake katika kijiji cha Lupaso katika maeneo ya Mtwara nchini Tanzania.
Akizungumza wakati wa ibada ya mazishi ya Mkapa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli, amewahimiza watanzania kujifunza kuishi maisha ya upendo na kuwatendea mema wengine.
Naye aliyekuwa Rais wa nne wa taifa hilo Jakaye Kikwete amemtaja mwendazake Mkapa kama kiongozi aliyechangia mengi nchini Tanzania kwa upando wake wa dhati yaliokuwa nao kwa taifa hilo.
Kwa upande wake Mwanasiasa mkongwe nchini humo Hassan Mwinyi amewahimiza watanzania na mataifa yote ya afrika mashariki kushirikiana katika kujenga amani katika mataifa hayo.
Marehemu Mkapa alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 81 katika hospitali kuu ya Dar-es-salam baada ya kuugua kwa mda mfupi.