Picha kwa hisani –
Nyanja ya filamu nchini inaomboleza kufuatia kifo cha muigizaji chipukizi Kenneth Magawe huku baadhi ya marafiki na waigizaji wenzake kwenye mitandao ya kijamii wakitaka kampuni za filamu kuwalinda wanachama wao.
Muigizaji huyo anaripotiwa kufariki usiku wa Jumamosi, Januari 30, baada ya kuvamiwa na kundi la majambazi akielekea nyumbani. Magawe alikuwa anaelekea nyumbani akitokea kurekodi filamu mpya ijayo ambapo aliagizwa na wezi hao kusalimisha mali yake yote ya thamani. Duru hiyo pia ilidokezea kuwa Magawe, ambaye ni mkazi wa mtaani Kasarani, alionekana kumtambua mmoja wa wezi hao na kumuita jina lake.
Kurasa za mitandao jamii za Magawe, zinaonyesha kwamba alikuwa bado anaazimia kunawiri kwenye ulingo wa uigizaji na pia muziki huku akijitambua kama muimbaji na pia mtunzi wa nyimbo lakini ni huzuni kubwa kuwa Mkenya huyo chipukizi mwenye talanta amekatiziwa ndoto yake na wahalifu ambao hawathamini maisha ya kijana mwenzao.