Story by Mimuh Mohamed-
Kamati ya pamoja ya bunge la kitaifa na seneti kuhusu usalama imeidhinisha uteuzi wa Japhet Koome kuwa Inspekta Jenerali wa Polisi nchini.
Mwenyekiti wa usalama wa kitaifa wa Seneti, ulinzi na uhusiano wa kitaifa William Cheptumo amewasilisha ripoti ya kamati hiyo bungeni kujadiliwa akipendekeza bunge kuidhinisha uteuzi wa Koome.
Akitoa hoja ya kujadili ripoti hiyo, Seneta wa Kisumu Tom Ojienda alimtaja Koome kama mtu aliyehitimu na mwenye elimu, huku Seneta wa Nyamira Okong’o Omogeni akisema Koome ana taaluma ambayo italeta mageuza katika idara ya Polisi.
Koome anachukua nafasi ya Hillary Mutyambai aliyejiuzulu kutoka na sababu za kiafya huku Koome akitarajiwa kulipiga vita swala la ufisadi katika idara ya usalama, uimarishaji utendakazi wa polisi miongoni mwa maswala mengine.