Picha kwa hisani –
Bunge la kaunti ya Taita taveta limetakiwa kufuatilia kwa karibu mno matumizi ya fedha za umma katika Serikali ya kaunti hiyo ili kuzuia ufisadi.
Seneta wa Taita taveta Johnes Mwaruma amesema bunge hilo halina sababu ya kulalamika na badala yake kuhakikisha fedha zilizotengewa maendeleo katika kaunti hiyo zinatumika vyema.
Mwaruma amelitaka bunge la kaunti hiyo kutekeleza majukumu yake vyema, akisema bila ya kuwepo na uwazi katika Serikali ya kaunti hiyo, basi wkaazi watakosa manufaa ya ugatuzi.
Wakati uo huo amewataka wakaazi wa kaunti hiyo kutohofia kuwasilisha maswala muhimu ya utendakazi wa kaunti hiyo na ambayo wanayatilia shaka.