Picha Kwa Hisani –
Kamati ya bunge la seneti inayoshughulikia janga la Corona imehairisha kikao cha kuwahoji maafisa mamlaka ya kusambaza vifaa vya matibabu nchini KEMSA baada ya afisa mkuu mtendaji wa mamlaka hio Jonah Manjari kukosa kufika mbele ya kamati hio.
Mwenyekiti wa kamati hio amemuamuru Manjari kuwasilisha barua rasmi kufikia saa nane mchana inayoonyesha kwamba ni mgonjwa akisema barua alioiwasilisha awali katika ubunge hilo haina uthibitisho,akisema kikao hicho kitafanyika juma lijalo.
Awali seneta Narok Ledama ole Kina amesema kikao hicho hakiwezi kuendeleza bila kuwepo kwa afisa huyo akisema kuna haja ya hatua kali za kisheria kuchukuliwa dhidi yake ikiwemo kutozwa faini ya laki tano na kutolewa agizo la kutiwa nguvuni kwani amekosa kuheshimu bunge la seneti.
Juma lilipota Manjari pamoja na mkurugenzi wa biashara wa KEMSA Eliud Muriithi na mkurgenzi wa kitengo cha zabuni katika mamlaka hio Charlse Juma walisimamishwa kwa kazi kwa madai ya kutoa zabuni za kusambaza vifaa vya kujikinga na corona kwa kaunti kwa njia isio ya halali na kufuja fedha za umma.